Jumatano 2 Julai 2025 - 14:19
Maulamaa wa Uturuki watangaza kumuunga Mkono Ayatollah al-Udhma Khamenei

Hawza/ Maulamaa wa Ahlul Bayt wa Uturuki wametangaza kwa kusema: Sisi Waislamu wenye ghera na waumini duniani, kamwe hatutakaa kimya mbele ya vitisho na dharau za Rais wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, bali tutaitetea kwa nafsi zetu zote hadhi tukufu ya uongozi wa Kiislamu, na tutawafanya maadui wa Uislamu na uongozi huo wajute.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza,Jumuiya ya Maulamaa wa Ahlul Bayt wa Uturuki katika taarifa yao wamesema: Sisi Waislamu wenye ghera na waumini duniani, kamwe hatutakaa kimya mbele ya vitisho na dharau za Rais wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, bali tutazitetea kwa nafsi zetu zote, hadhi tukufu ya uongozi wa Kiislamu, na tutawafanya maadui wa Uislamu na uongozi huo wajute.
Matini ya taarifa hii ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mvunja nguvu za madhalimu

Ukafiri wote dhidi ya Imani yote!

Katika historia yote, kuanzia kwa Nabii Adam (as) hadi leo, kambi ya haki na batili daima zimekuwa zikipambana, na leo pia, ukafiri wote umepanga safu dhidi ya imani yote, na pambano hili linaendelea kwa nguvu zote.

Kambi ya ubeberu, chini ya uongozi wa shetani mkubwa — Marekani — kwa kutumia vyombo vya habari na silaha za kisasa, inajitahidi kuyafanya mataifa mengine, hasa ya ulimwengu wa Kiislamu, yajisalimishe kikamilifu na kuwa watumwa wao.

Wakati mapambano katika medani ya Ghaza, Lebanon, Yemen na Iran yanaendelea, matusi, mashambulizi na vitisho dhidi ya vitu vitukufu vya Uislamu na Waislamu pia vimefikia kilele.

Mfano wa hivi karibuni ni vitisho vya kihuni dhidi ya Kiongozi wa Waislamu, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na mstari wa mbele wa mapambano — Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Mola amuhifadhi) — kutoka kwa rais mjeuri na mpumbavu wa Marekani muuaji, pamoja na Wazayuni.

Sisi Maulamaa wa Ahlul Bayt wa Uturuki tunalaani vikali mashambulizi haya ya kihuni na vitisho hivyo, na tunawalingana Waislamu wote pamoja na wanyonge wa dunia kuilinda dini yao, utukufu wao, heshima na hadhi yao.

Uislamu, Qur'ani, Mtume, vitu vyote vitakatifu, na viongozi wetu ni mistari myekundu kwetu. Kuwalenga ni sawa na kupambana na Waislamu wote duniani.

Waislamu wenye ghera na waumini duniani, kamwe hawatakaa kimya mbele ya vitisho hivi na dharau hizi, bali kwa nafsi zao zote watatetea vitukufu vyao na hadhi tukufu ya uongozi wa Kiislamu, na kwa idhini ya Allah Mtukufu, watawafanya maadui wa Uislamu na wa wilaya wajutie.

والسلام علی من اتبع الهدی

Jumuiya ya Maulamaa wa Ahlul Bayt wa Uturuki
(Ahladar)
1 Julai 2025
Istanbul

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha